Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mimi mwenyewe nilibakwa, nikaanza kuwasaidia wanawake wengine-Ashura Msiteka

Mimi mwenyewe nilibakwa, nikaanza kuwasaidia wanawake wengine-Ashura Msiteka

Pakua

Ulimwengu ukiwa katika siku 16 za kuhamasisha kupinga ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake na wasichana, takwimu zinaonesha kuwa wakati huu wa janga la COVID-19, wanawake wengi zaidi wamedhulumiwa kwa namna moja au nyingine. 

Sasa kikundi cha Coalition of grassroots women initiative kilicho mtaa wa Dandora mjini Nairobi kimekuwa kikiwahudumia wanawake na wasichana ambao wanapitia ukatili wa aina tofauti. Kiongozi wa kikundi hiki Ashura Msiteka ambaye mwenyewe ni manusura wa ukatili  amezungunza na mwandishi wa Kenya Jason Nyakundi kuhusu shughuli zao.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Jason Nyakundi
Audio Duration
3'17"
Photo Credit
© Julius Mwelu/ UN-Habitat