Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wazee wazungumza historia ya mafuriko kwenye Ziwa Albert

Wazee wazungumza historia ya mafuriko kwenye Ziwa Albert

Pakua

Maelfu ya watu wanendelea kuathiriwa na mafuriko yanayoshuhudiwa katikaa meneo mbalimbali hasa yale ya Ziwani nchini Uganda.

Licha ya onyo kutoka kwa serikali na asasi za kiraia kuwa mafuriko haya yanaweza kuendelea, mpaka sasa baadhi ya watu wanahama mita chache wakiwa na matumaini kwamba maji haya yatapungua mambo yarejee kama kawaida.

Hata hivyo, watu wa asili kwenye Ziwa Albert wanaonya kuwa mambo bado kutokana na mfano kama huo ulioshuhudiwa na waliokuwepo miaka ya elfu moja kendamia sitini.

Je, ilikuwaje? Nani ni mwathirika zaidi mwaka huu kati ya wenyeji na wahamiaji?

Pata taarifa zaidi katika mahojiano baina ya John Kibego na Mzee Baranaba Bagadira Kakura wa ufukwe wa Wanseko katika wilaya ya Buliisa

Audio Credit
Anold Kayanda/ John Kibego
Audio Duration
3'58"
Photo Credit
UN News/ John Kibego