Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikopo ya bodaboda yageuka kaa la moto kutokana na COVID-19 Uganda

Mikopo ya bodaboda yageuka kaa la moto kutokana na COVID-19 Uganda

Pakua

Nchini Uganda, serikali ilipatia vijana mikopo ili kuwawezesha kujinasua kiuchumi na hivyo kuwa sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Hata hivyo mafuriko katika Ziwa Albert na mlipuko wa ugonjwa wa Corona, COVID-19 vimevuruga uwezo wa vijana kurejesha mkopo huo. Sasa vijana kupitia vyongozi wao wanaomba serikali kutotumia mkono wa sheria dhidi ya wanaopata matatizo kuzingiatia ratiba ya ulipaji wa fedha walizopatiwa. Viongozi wa kisiasa wanaunga mkono ombi la vijana la kuelewa hali yao lakini wataalamu wa maendeleo ya  jamii wanasema, pesa hizo ni lazima zilipwe. Je, itakuwaje? Basi ungana na John Kibego katika makala ifuatayo ili kufahamu kwa undani. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'40"
Photo Credit
UN News/ John Kibego