Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tulianzisha shirika la mazingira ili kupambana na uchafu na ukosefu wa ajira-Sam Dindi  

Tulianzisha shirika la mazingira ili kupambana na uchafu na ukosefu wa ajira-Sam Dindi  

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya choo duniani, Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, linaeleza kuwa Ulimwenguni, asilimia 80 ya maji taka yanayozalishwa na jamii yanarudi katika mzunguko wa ikolojia bila kusafishwa,  na vilevile taka mwili za binadamu zisizodhibitiwa mathalani kwa kuwekewa dawa za kuua vijidudu, huingia kwenye mazingira na kueneza magonjwa hatari na sugu.   

Matumizi salama ya taka za binadamu husaidia kuokoa maji, hupunguza na hunasa hewa chafuzi chafuzi ili zitumike katika uzalishaji wa nishati na kukipatia  kilimo chanzo cha kuaminika cha maji na virutubisho. Takwimu za FAO zinaeleza kuwa hivi leo, watu bilioni 4.2 wanaishi bila mazingira bora ya kujisafi badala yake mara nyingi hutumia vyoo visivyoaminika, visivyo vya kutosha au wanajisaidia haja kubwa katika maeneo ya wazi.  

Ni katika hali kama hiyo ambapo vijana nchini Kenya, mnamo mwaka 2012, waliamua kuanzisha shirika la Mazingira Yetu na limekuwa katika mstari wa mbele kuwaleta vijana pamoja katika harakati za kusafisha mazingira na kuhamasisha watu kuwa na vyoo na kuyadhibiti maji taka. Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amemhoji Mkurugenzi na ambaye ni mmoja wa waasisi wa shirika hili Bwana Sam Dindi. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Jason Nyakundi
Audio Duration
4'31"
Photo Credit
Picha ya maktaba ya UM