Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto kuzaliwa njiti si mkosi, akipatiwa matunzo anakua- Doris Mollel

Mtoto kuzaliwa njiti si mkosi, akipatiwa matunzo anakua- Doris Mollel

Pakua

Kila mwaka takribani watoto milioni 15 wanazaliwa njiti, yaani ujauzito ukiwa haujatimiza wiki 37. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO ambalo linasema kuwa idadi inaongezeka. Kuzaliwa njiti ni moja ya sababu ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 na leo katika kuadhimisha siku ya kuhamasisha umma kuhusu watoto njiti, wito unatolewa ili kusaidia zaidi watoto hao. Taasisi ya Doris Mollel nchini Tanzania imejikita katika kusaidia watoto njiti kwa kuzingatia kuwa Mkurugenzi Mtendaji mwenyewe Doris alizaliwa njiti akiwa na uzito wa gramu 900. Hatua zake zimemfikisha hadi kwa wakimbizi na Laurean Kiiza wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC, Dar es salaam nchini Tanzania amezungumza naye kufahamu alikoanzia na matarajio ya baadaye.

Audio Credit
Anold Kayanda/ Laurean Kiiza
Audio Duration
5'28"
Photo Credit
Doris Mollel Foundation.