Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA na harakati zake za kuhakikisha huduma ya afya ya uzazi kambini

UNFPA na harakati zake za kuhakikisha huduma ya afya ya uzazi kambini

Pakua

Wakati mkimbizi anajikuta ukimbizini, mahitaji yake yanakuwa ni mengi lakini kwa mazingira aliyonayo anajikuta akitegemea msaada wa kibinadamu kutoka mashirika. Mara nyingi hutokea kwamba mahitaji ambayo yanapewa kipaumbele ni yale ya msingi ikiwemo maji, chakula na huduma za kujisafi. Hata hivyo huduma ya afya na hususan afya ya uzazi inakuwa ni moja ya mahitaji muhimu hususan kwa mama na mtoto.

Katika kuhakikisha kwamba wanawake hata walio kambini wanapata huduma hizo shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA imetoa mafunzo kwa wakunga ambao wako katika vituo saba ndani ya kambi ya Nyargusu, mkoa wa Kigoma nchini Tanzania. Basi ungana na Stella Vuzo afisa wa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam, UNIC katika mahojiano na Dkt. Sande Rwebangira kutoka kitengo cha afya ya uzazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA ambaye anaanza kwa kuelezea hali ya wakunga kambini ikoje.

Audio Credit
UN News/Stella Vuzo
Audio Duration
6'25"
Photo Credit
UN