Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii yetu imenufaika sana na matangazo ya redio za kijamii.

Jamii yetu imenufaika sana na matangazo ya redio za kijamii.

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya redio duniani ambapo ulimwengu unakiangazia chombo hicho ambacho kwa miongo mingi kimekuwa muhimu kupitisha taarifa muhimu kwenda kwa jamii na pia kuwapa wanajamii fursa ya kueleza mawazo yao katika ujenzi wa maisha yao, Umoja wa Mataifa umeamua maadhimisho ya mwaka huu yalenge kuzienzi redio za kijamii ambazo zinatoa fursa kwa watu walioko mashinani. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, Audrey Azoulay katika kuadhimisha siku hii ya radio duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 13 mwezi Februari anasema mbinu tofauti za kusambaza taarifa kupitia radio iwe ni katika mita bendi ya AM au FM au kwa kupitia teknolojia za kidijitali au kwenye wavuti zinaendana na utofauti katika yaliyomo kwenye programu ambazo zinazalishwa na wingi wa maoni, utamaduni na yale yanayotangazwa. Kupitia makala hii, wasikilizaji wa redio hizo huko wilayani Pangani, Tanga Tanzania wanaeleza walivyonufaika nazo.  

Audio Credit
UN News
Audio Duration
3'28"
Photo Credit
UN /MINUSCA