Vituo vyetu vya msaada wa sheria huanzishwa kwa kuzingatia mahitaij yaliyopo- WLAC

30 Julai 2019

Nchini Tanzania kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake, WLAC kimekuwa msaada hasa kwenye maeneo ambako bado kuna changamoto kuhusu haki na sheria. WLAC ikiwa inatekeleza majukumu yake katika wilaya 23 za mikoa ya Tanzania inalenga makundi tofauti tofauti hususan wanawake ikiwa ni katika kutekeleza lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu amani, haki na taasisi thabiti. Flora Nducha alizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, Wakili Theodosia Muhulo-Nshala ili kuweza kufahamu ni misingi ipi huzingatiwa katika kuanzisha vituo hivyo? Wakili Theodosia anaanza kwa kuzungumzia kituo kilichopo wilayani Muleba mkoani Kagera.

 

Audio Credit:
Assumpta Massoi/Flora Nducha
Audio Duration:
4'15"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud