Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kaunti ya Nairobi na harakati za kulinda mazingira

Kaunti ya Nairobi na harakati za kulinda mazingira

Pakua

Mji wa Nairobi, nchini Kenya ni kati ya miji inayokua kwa kasi zaidi barani Afrika, lakini suala la mazingira limekuwa changamoto kubwa. Kuanzia uzoaji taka, mifumo ya maji taka na hata ubora wa hewa ni baadhi ya changamoto zinazokumba mji huu. Idadi ya watu inazidi kuongezeka kila kukicha lakini miundo mbinu ya mazingira ni ile ile ya miaka nenda miaka rudi. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi alipata fursa ya kuzungumza na afisa mkuu wa idara ya mazingira na mali asili katika serikali ya kaunti ya Nairoiabi David Makori ili kufahamu hali ya sasa na kile ambacho kinafanyika ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama. Bwana Makori anaanza kwa kuelezea hali ya sasa ya mji wa Nairobi kimazingira.

Soundcloud
Audio Credit
Flora Nducha/ Jason Nyakundi/ David Makori
Audio Duration
4'31"
Photo Credit
Julius Mwelu/UN-Habitat