Ni muhimu tutatue kiini cha vijana kushiriki ngono katika umri wa hata miaka tisa-NAYA Kenya

24 Julai 2019

“Ukweli ni kwamba vijana kuanzia umri wa miaka tisa wanashiriki vitendo vya ngono,” hiyo ni moja ya kauli ya Robert Aseda, kijana kutoka Kenya akiwakilisha asasi ya kiraia kutoka Kenya iitwayo mtandao wa barubaru na vijana Afrika, NAYA.

Akizungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Kijana Aseda amesema licha ya kwamba jamii inalifumbia macho suala la kwamba vijana kuanzia umri mdogo wanamahusiano ya kingono iwe na watu wa umri wao au na watu walio wazidi umri kwa ajili ya sababu mbali mbali lakini ukweli ni kwamba hiyo ni changamoto na hatua stahiki zinapaswa kuchukuliwa.

Basi ambatana na mwakilishi huyu wa NAYA Kenya alipohojiwa mapema mwaka huu kandoni mwa kongamano la vijana mapema mwaka huu hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani

Audio Credit:
Arnold Kayanda/Grace Kaneiya/Robert Aseda
Audio Duration:
3'56"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud