Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchafuzi wa Mto Kafu na athari zake wamulikwa, Uganda

Uchafuzi wa Mto Kafu na athari zake wamulikwa, Uganda

Pakua

Maeneo oevu ni sehemu muhimu katika suala zima la uhifadhi wa mazingira ambalo linapigiwa chepuo katika Malengo ya maendeleo endelevu (SDGS) hususani lengo namba 15, linalohimiza uhifadhi wa mazingira yakiwemo maeneo oevu  pamoja na matumizi endelevu ya misitu na kuzuia kuenea kwa hali ya jangwa.

Tishio la uchafuzi wa mazingira linazikabili nchi nyingi duniani ikizingatiwa kuwa ni kichochea cha mabadiliko ya tabianchi ambapo pia katika lengo namba 13 la agenda ya maendeleo ya mwaka 2030 hatua za dharura zinahitajika ili kudhibiti mabadiliko haya ya tabianchi na athari zake.

Nchini Uganda mto Kafu ni miongoni mwa maeneo muhimu sana ambayo sasa yanakabiliwa na uchafuzi mkubwa kutokana na shughuli za binadamu hali ambayo inaweka hatarini sio tu mustakabali wa mto huo bali pia wa wanachi wa eneo hilo. Mwandishi wetu John Kibego nchini humo amevinjari katika mto huo ili kutanabaisha hali halisi na atahri za uchafuzi huo kwa maisha ya binadamu, kipato na uhai wa viumbe vya majini. Kwa undani zaidi ungana naye katika makala ifuatayo.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
4'30"
Photo Credit
IOM/Amanda Nero