Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana kukamatwa juu ya mkopo wa serikali, Uganda

Vijana kukamatwa juu ya mkopo wa serikali, Uganda

Pakua

Katika harakati za kuhakikisha kwamba vijana wanapata ajira sio tu kwa kuajiriwa lakini kwa pia kwa kujiajiri kupitia ubunifu wa biashara mbali mbali, serikali zimeanza kuchukua hatua na kuweka programmu ambazo zinatoa mikopo kwa vijana kwa mfano vikundi kwa ajili ya kufanya biashara.

Lakini kuna changamoto mbali mbali ambazo bado zinakwamisha vijana katika ubunifu huo na kufanya biashara ambazo zinazaa matunda.

Darubini yetu imelenga nchini Uganda leo ambako katika makala hii ya John kibego ametuletea maoni ya wadau kadha wa maendeleo ya vijana wakati ambapo viongozi wa serikali wanaohusika na maendeleo ya jamii wanaangazia uimarishaji wa hatua za kuwakamata vijana waliotumia visivyo fedha walizopokea chini ya mradi wa kukwamua vijana nchini humo wa Youths' livelihood Programme iliyoanzishwa miaka 6 iliyopita.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
FAO/Giulio Napolitano