Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa Uchimbaji visima vya maji masafi ni mkombozi kwa wengi Juba- UNICEF

Mradi wa Uchimbaji visima vya maji masafi ni mkombozi kwa wengi Juba- UNICEF

Pakua

Umoja wa Mataifa na washirka wake kupittia miradi mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele kutoa usaidizi hasa kwa wanawake na watoto walioko katika  maeneo ya migogoro ya kivita.

Miongoni mwa misaada hiyo ni huduma ya maji ambayo ni bidhaa adimu kutokana na vita, ukame na pia mabadiliko ya tabianchi. Mji wa Juba nchini Sudan kusini  ni moja ya miji inayokuwa na tatizo kubwa la maji lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kupitia mradi wa uchimbaji visima vya maji safi katika maeneo yenye migogoro, umeendelea kuwa mkombozi kwa jamii na hususani wanawake wanaokabiliwa sio tu na  vitendo vya ubakaji wakati wakienda mbali kuchota maji, bali pia changamoto za  maji machafu kwa ukosefu wa miundombinu stahiki katika  jamii hizo .Mradi wa mpya wa maji umeleta nuru na kuwapunguzia adha wanawake hao.

Bi Charity na watoto wake wamekuwa wanufaika wa mradi  huo wa UNICEF. Je wanataka kujua wamenufaikiaje? Kwa undani zaidi Ungana na mwandishi wetu Patrick Newman na Bi Charity  katika makala hii.

 

Soundcloud
Audio Credit
Flora Nducha/ Patrick Newman
Audio Duration
3'13"
Photo Credit
Photo: IRIN/A. Morland