Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wataka nafasi katika vyombo vya habari ili kustawi, Uganda

Wanawake wataka nafasi katika vyombo vya habari ili kustawi, Uganda

Pakua

Nafasi ya mwanamke iwe katika siasa, uchumi au masuala mengine ya kijamii ni muhimu sana sio tu kwa kumuinua na kumuwezesha mwanamke lakini pia katika kuendeleza jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Hivi sasa ajenda ya maendeleo endelevu au SDGs  ya mwaka 2030, inapigia chepuo uwezeshaji wa wanawake katika kila njia kupitia lengo namba 5. Na nchi mbalimbali zimeanza kuitikia wito huo japo bado kuna baadhi ya nchi mwanamke hana sauti na mchango wake hauthamininiwi.

Nchini Uganda, wanawake wanahabari na wanasiasa wamelivalia njugu suala hilo muhimu na kutaka nafasi muhimu katika usimamizi wa majukumu mbalimbali ikiwemo usimamizi wa vombo vya habari pamoja na kutoa nafasi kwa wanawake wanasiasa kutumia vyombo hivyo ili waongeze umahiri katika jamii na vilevile kipato.  Kwa undani zaidi hii hapa makala iliyoandaliwa na mwandishi wetu nchini humo, John Kibego.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Sauti
3'58"
Photo Credit
Picha ya UNAMID/ Hamid Abdulsalam