Kampeni kuhusu nishati endelevu yashika kasi, Uganda

25 Julai 2019

Nishati endelevu ni suala ambalo linatathminiwa katika juhudi za kupambana na uchafuzi wa mazingira na athari zake duniani kote. Hili pia linapigiwa chepuo katika lengo namba saba la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs au agenda ya 2030.

Nchini Uganda serikali na wadau wake wanaendesha kampeni kubwa katika,maeneo mbalimbali ya taifa hilo la afrika Mashariki ili kuhakikisha kwamba mtazamo wa jamii kuhusu matumizi ya  teknolojia ya nishati endelevu unabadilika lengo likiwa kuhakikisha kwamba wanakumbatia matumizi yake ikiwemo paneli za sola na majiko yasiotumia mkaa mwingi kupika.Ili kupata undani wa kampeni hiyo ungana na mwandishi wetu John Kibego katiak makala ifuatayo.

Audio Credit:
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration:
3'48"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud