Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Picha ya UN

PADI Ruvuma nchini Tanzania yasaidia utekelezaji wa lengo namba 10 la SDGs

Shirika la kiraia la PADI lenye lengo la kusaidia watu maskini na wenye ulemavu, limekuwa chachu ya maendeleo kwa wazee kwenye manispaa ya Songea mkoani Ruvuma nchini Tanzania. Shirika hilo limepanua mawanda yake ya usaidizi na kugusa maisha ya wazee kwa lengo la kusaidia waondokane na utegemezi na hivyo kuinua kipato chao sambamba na lengo namba 10 la malengo ya maendeleo endelevu la kupunguza pengo la kipato na hivyo kumkwamua mtu kiuchumi, Je PADI inafanya nini? John Kabambala wa radio washirika Kidstime FM amefunga safari hadi kwenye manispaa hiyo na kuzungumza na mmoja wanufaika bi.

Audio Duration
3'49"
Special Olympics

Sada Nahimana mfano dhahiri wa manufaa ya michezo

Michezo kwa amani na maendeleo ni kaulimbiu ambayo iko bayana katika malengo ya maendeleo endelevu ikimaanisha kuwa michezo inasaidia siyo tu kuongeza kipato bali pia kuleta utangamano kwa jamii na pia kuboresha maisha ya watu. Hii imedhihirika hasa kwa vijana hususan nchini Burundi.

Sauti
3'52"
Photo: UN Women/Ryan Brown

Wanawake wanaopigania haki wanasimamia kazi yao-Bi. Bisimba

“Wanawake labda kwa makuzi yao, wakifanya kitu wanafanya kwa kumaanisha,” hii ni sehemu ya maneno yake Helen Kijo Bisimba, mwanaharakati nguli wa kupigania haki za binadamu nchini Tanzania. Akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii Bi. Bisimba amesema wanawake ambao wanajihusisha na kupigania haki, ni kwa sababu wamepitia changamoto zitokanazo na ubinyaji wa haki na wanasimamia kazi yao. Basi ungana na Flora Nducha na Bi Kijo  kwa undani zaidi.

Sauti
3'38"
UN News/ Anton Uspensky

Athari za mabadiliko ya tabianchi hazina mipaka- mkaazi Bunyoro-Uganda

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linachagiza mataifa kuchukua hatua za haraka ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Lengo hilo limeorodhesha malengo madogo ambayo yatasaidia katika kufanikisha SDG 13 ifikapo mwaka 2030. Katika kupima utekelezaji wa lengo hilo, moja ya hatua ni kuimarisha uwezo wa kupanga na kusimamia mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika nchi maskini, visiwa vidogo na zile zinazoendelea, ikiwemo kwa kulenga wanawake,vijana na jamii mashinani na zilizotengwa.

Sauti
3'41"
ONU Info/Florence Westergard

Kutokata tamaa na UNHCR vimenifikisha hapa nilipo:Mkimbizi Bahige

Hadhi ya ukimbizi mara nyingi si hiyari bali changamoto na mazingira hulazimisha mamilioni ya watu kila uchao kufungasha virago na kukimbia patakapowasitiri. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa wengi maisha yao huishia makambini, baadhi hukumbatiwa na jamii wakimbiliako, wengine huzogomwa na mitihani na wachache kama mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Rawhide jimboni Wyoming hapa Marekani, Bertine Bahige hupata fursa ya kupelekwa taifa la tatu kupitia mpango maalumu wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR.

Sauti
4'39"
UNIDO

Kijana kutoka Tanzania atumia stadi alizozipata kuwezesha vijana wenzake

Lengo namba nane la malengo ya maendeleo endelevu SDGs ya Umoja wa Mataifa linaangazia uchagizaji wa ukuaji uchumi endelevu na jumuishi na ajira yenye matokeo na kazi inayozingatia utu kwa wote.Katika kuangalia hatua zilizopigwa kufikia lengo hilo, takwimu zinaonyesha kuwa ukosefu wa ajira ulikuwa ni asilimia 5.7 mwaka 2016 huku idadi ya wanawake wasio na ajira ikiwa ni zaidi ya wanaume katika umri mbali mbali.

Sauti
4'47"
ITU

Tanzania inajitahidi kujumuisha wanawake katika TEHAMA: Injinia Ichokeleza

Sekta ya habari na mawasiliano kwa muda mrefu hasa kwenye mataifa yanayoendelea imekuwa ikitawaliwa na wanaume. Lakini katika zama hizi za utandawazi na umuhimu wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayohimiza yeyote asiachwe nyuma na treni ya maendeleo ya 2030. Nchi zimeanza kuchukua hatua kwa chagizo la Umoja wa Mataifa kujumuisha wanawake katika TEHAMA. Nchini Tanzania serikali imeweka mikakati ikihusisha kuhamasisha jamii wakiwemo wazazi kuwachigiza watoto wao wa kike kuingia katika masomo yahusianayo na TEHAMA.

Sauti
4'49"
Picha: IFAD/GMB Akash

Kijana na ajira nchini Tanzania

Nchini Tanzania kijana Richard Hamisi baada ya kuhitimu shahada yake ya biashara na fedha katika Chuo Kikuu Mzumbe, mwaka jana wa 2018, ameandika wazo la kuanzisha maghala ya kutunzia nafaka katika maeneo yanayozalisha mazao mengi nchini huko kama njia mojawapo ya kuhakikisha mazao yanatunzwa vyema na hivyo uhakika wa chakula na bei nzuri  ya mazao. Akihojiwa na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam, Richard amefafanua kuhusu maghala hayo na kwanza anaanza kwa kueleza alivyopata wazo la kuanzisha mradi huu.

Sauti
2'9"
UN News/Nam Cho

Mada kwa kina- Biashara mtandao

Ijumaa ya leo mada kwa kina inamulika biashara  mtandao na manufaa yake kwa jamii hivi sasa hususan zile ambazo wakazi wake wanatumia simu za mkononi na wana uwezo wa kupata mtandao wa intaneti unaowaunganisha kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram na Twitter. Grace Kaneiya amefuatilia kwa kina hali ilivyo Afrika Mashariki hususan Kenya, Tanzania na Uganda na wapigaji chepuo mada hii UNCTAD ambayo ni kamati ya biashara na  maendeleo ya Umoja  wa Mataifa. Karibu!

Sauti
7'39"