Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaharakati wakemea wanawake kuvuliwa nguo hadharani Uganda

Wanaharakati wakemea wanawake kuvuliwa nguo hadharani Uganda

Pakua

Ukatili wa kijinsia ni jambo linaloleta hofu kubwa kwa jamii hususan wanawake na watoto wa kike. Ukatili huo ni wa aina mbalimbali ikiwemo wa kingono, kipigo na hata manyanyaso. Mathalani vitendo vya wanawake au wasichana kunyanyaswa kutokana na mavazi yao ni jambo ambalo limekuwa likiripotiwa mara kwa mara maeneo mbalimbali duniani na hivi karibuni matukio kama hayo yaliripotiwa Uganda lakini sauti zilipazwa. Nini kilifanyika? John Kibego ndiye shuhuda wetu.

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
3'31"
Photo Credit
YWCA Tanzania