Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Kuadhimisha Siku ya Maji duniani

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya maji ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni "maji na usalama wa chakula" inaonekana kuwa nchi nyingi zimepiga hatua katika udhibiti wa maji lakini bado juhudi zaidi zinahitajika.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova ameitaka dunia kuungana pamoja ili kuhakikisha kila mtu ana fursa ya maji safi na chakula, sasa na baadaye.

Kwa upande wake Wananchi ambao wengi hukabiliwa na matatizo ya maji wanasemaje kuhusu siku hii.

Hawa ni baadhi ya waakazi wa Afrika Mashariki.

Katika kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku

Takribani watu milioni 5 wenye umri wa miaka 30 na zaidi wamekufa kutokana na matumizi ya moja kwa moja ya tumbaku kote duniani, na hiyo ni sawa na kifo cha mtu mmoja kila baada ya sekunde sita.

Kwa mujibu wa ripoti  ya WHO maeneo ambayo yana kiwango kikubwa cha vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku ni Marekani na bara Ulaya ambako tumbaku imekuwa ikitumika kwa muda mrefu zaidi.

Pia ripoti hiyo imebainisha kwamba tumbaku ndio mihadarati pekee iliyohalalishwa ambayo inawaua watu wengi wanaoitumia kama ilivyokusudiwa na wazalishaji.

Mwanamke aliyejitolea kuwasaidia watoto wasichana na wanawake kwa jumla:Mukamabano

Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Wanawake duniani kuna wanawake mbali mbali wanaojitoa kusaidia wanawake wenzao na wasichana. Miongoni mwao ni Marie Claudine Mukamabano kutoka nchini Rwanda ambaye anaishi Marekani. Marie ameanzisha kituo cha kuwalea watoto yatima nchini Rwanda. Yeye ni manusura wa mauaji ya kimbari lakini pia ni mwanzilishi wa kituo cha kulea watoto kiitwacho "Why Do I Exist". Kituo hiki kinawasaidia watoto wasichana na wanawake. Amezungumza na Mkuu wa Idhaaa hii Flora Nducha. Wasikilize...

UM waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kupanda mlima Kilimanjaro

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na makundi mengine ya kiharakati pamoja na serikali ya Tanzania umeadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kupanda mlima kulimanjaro kama ishara mojawapo ya kusuma mbele nafasi ya mwanamke huku ikipinga vitendo vya dhulma dhidi yao.

Hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hilo, ambalo pia limewashirikisha vijana kutoka mataifa mbalimbali barani afrika waliopaza sauti zao juu ya kulinda haki za wanawake duniani kote.

Umuhimu na thamani ya mwanamke wa Kijijini

Wiki hii kwenye Umoja wa Mataifa kunafanyika kongamano ambalo linajumuisha wanawake kutoka kila pembe kujadili umuhimu na thamani ya kila mwanamke kijijini. Kongamano hili limeandaliwa na kitengo cha wanawake cha Umoja wa Mataifa UN WOMEN na linashirikisha wanawake viongozi na wanaharakati wa kupigania haki za wanawake na wadau wengine ambao wanachagiza haki za wanawake.

Kongamano la UM juu ya ukuzaji sekta ya madini lafikia tamati Tanzania

Kamishna ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya uchumi kwa kanda ya afrika, imehitimisha mkutano wake wa 16 jijini Dar es salaam ambako imesisitiza haja ya kuimarisha sekta ya madini kwa ajili ya kukuza maendeleo barani humo.

(SAUTI GEORGE NJOGOPA)

Mkutano huo ulioduma kwa muda wa juma moja, umewaleta pamoja mawaziri wa masula ya madini, watunga sera, wawakilishi kutoka nchi za Ulaya, pamoja na makundi mengine ya kimaendeleo.

Maoni kuhusu umuhimu wa Radio ya UM

UM ukiadhimisha siku ya Radio duniani hii leo watu kutoka Afrika wametoa maoni kuhusu umuhimu wa Radio, ikiwemo Radio ya Umoja wa Mataifa. Mwandishi wetu kutoka Tanzania alipata kuzungumza na watu mbali mbali waliotoa maoni tofauti tofauti kuhusu umuhimu wa radio ya Umoja wa Mataifa.

(MAONI KUTOKA TANZANIA)

Mahiga amefurahi sana kwa hatua ya kihistoria ya kuhamisha ofisi yake Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema Alhamisi kuwa amefurahi sana kufanikiwa kuhamisha ofisi yake kutoka mjini Nairobi Kenya na kuiweka mjini Moghadishu Somalia.

Katika waraka maalumu aliowaandikia Wasomali, Mahiga amesema anashukuru msaada mkubwa wa vikosi vya muungano wa Afrika AMISOM na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya siasa kwa ajili ya Somalia UNPOS kufanikisha hilo.

Tanzania inadai maili 350 katika bahari ya Hindi

Tanzania imewasilisha ombi la kuongeza eneo la maili 150 hadi 200 za eneo lililo chini ya udhibiti wake kwenye bahari ya Hindi.

Chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa sheria za bahari wa mwaka 1982, taifa lililo katika mwambao wa bahari lina haki ya kudai eneo ili kuweza kutafuta mali asili kama samaki, madini na mafuta.

Ombi hilo limewasilishwa kwenye Umoja wa Mataifa kwa wahusika wa masuala ya bahari na aliyewasilisha ombi hilo ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi wa Tanzania Profesa Anna Tibaujuka.