Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahiga amefurahi sana kwa hatua ya kihistoria ya kuhamisha ofisi yake Somalia

Mahiga amefurahi sana kwa hatua ya kihistoria ya kuhamisha ofisi yake Somalia

Pakua

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema Alhamisi kuwa amefurahi sana kufanikiwa kuhamisha ofisi yake kutoka mjini Nairobi Kenya na kuiweka mjini Moghadishu Somalia.

Katika waraka maalumu aliowaandikia Wasomali, Mahiga amesema anashukuru msaada mkubwa wa vikosi vya muungano wa Afrika AMISOM na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya siasa kwa ajili ya Somalia UNPOS kufanikisha hilo.

Ameongeza kuwa hii ni hatua ya kihistoria kwani mwakilishi wa mwisho wa Umoja wa Mataifa kuwepo ndani ya Somalia ni James Victor Gbeho ambaye aliondoka Somalia mwaka 1995.

Mahiga amesisitiza kuwa kuwepo ndani ya ardhi ya Somalia kutasaidia kuwa karibu na wadau wote, serikali ya mpito, uongozi mwingine, jumuiya za kijamii, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanya biashara, waandishi habari na Wasomalia wa kawaida. Amesema hali hiyo itawasaidia kuelewana zaidi na kufanya kazi pamoja katika kipindi hiki muhimu.

(SAUTI YA AGUSTINE MAHIGA)