Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Nchi nyingi masikini hazijapa suluhu ya malaria

Wakati ulimwengu umeadhimisha siku ya Malaria bado nchi hasa zilizo maskini hazijapata suluhu kamili na njia mwafaka za kupambana na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.

Bado watu wengi hawana uwezo au hawajapata hamasisho kuhusu njia kamili za kujikinga kutokana na ugonjwa wa Malaria ugonjwa ambao husababisha vifo vingi zaidi kwenye nchi hizi.

Ukosefu wa madawa ya kutibu ugonjwa wa malaria na neti za kujikinga dhidi ya mbu pamoja na madawa ya kutibu neti hizo ni baadhi ya masuala yanayoyatia hatarini maisha ya watu wengi kila siku.

Gharama kubwa na huduma duni ni tatizo kwa afya ya jamii

Leo ni siku ya afya duniani, Umoja wa Mataifa waungana na dunia kuadhimisha siku hii ambayo kwa mwaka huu inajikita kupiga darubini masuala ya afya na uzee.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa na afya njema ni chachu ya watu kuishi maisha bora na marefu kwa faina ya familia na jamii zao.

Hata hivyo imekuwa ni mtihani mkubwa kwa watu hasa kutoka nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo umri wa watu kuishi unakadiriwa kutozidi miaka 50.