Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wakimbizi wa maziwa makuu Tanzania waanza warejea nyumbani

Wakati dunia hii leo inaadhimisha siku ya wakimbizi ambako kunasisitizwa kuepusha madhira yanayoweza kuzalisha watu wa jamii hiyo, idadi kubwa ya wakimbizi kutoka eneo la maziwa makuu sasa wameanza kurejea nyumbani baada ya kuwa uhamishoni kwa kipindi kirefu

Huko nchini Tanzania ambako kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikihifadhi wakimbizi kutoka nchi za Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Somalia ripoti zinaonyesha kuanza kupungua kwa idadi ya wakimbizi hao walikubali kurejea makwao.

Kutoka Dar es salaam George Njogoa anaripoti zaidi

IOM yaendelea kuahamisha wakimbizi wa Sudan Kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanzisha shughuli ya kuwahamisha wakimbizi kutoka kituo cha Al Damazin kilicho kwenye eneo la magharibi kati ya mpaka wa Ethiopia na Sudan kwenda kambi mpya iliyo eneo la Benishangul Gumuz kaskazini magharibi mwa Ethiopia.

Uamuzi wa kuhamisha wakimbizi hao ulifanywa baada ya kituo hicho ambacho kina uwezo wa kuwahifadhi watu 14,000 kufurika.

Duru ya mwisho mjadala wa Rio+20 imeanza Brazil

Majadiliano ya matokeo ya mwisho ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo endelevu au Rio+20 yako yako katika hata za mwisho.

Majadiliano hayo yanaanza rasmi Juni 20 hadi 22 mjini Rio Dejaneiro Brazili ambako wakuu wan chi na serikali mbalimbali wanatarajiwa kutia saini nyaraka muhimu kwenye mkutano huo.

Mkutano huo pia unahudhuriwa na makundi mbalimbali, wakiwemo wadau wa maendeleo, jumiya ya kidini, wawakilishi wa jumuiya za kijamii na mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s.