Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Mradi wa maji waleta nuru kambi ya Dadaab

Kambi ya Dadaab iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya inahifadhi wakimbizi kutoka Somalia. Kambi hii inaelezwa kuwa ni kubwa kuliko kambi zote za wakimbizi duniani ikiwa inahifadhi wakimbizi zaidi ya Laki Nne na Nusu. Uhaba wa maji umekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo. Lakini nuru imechomoza na kubadili maisha ya familia za kifugaji. Ni nuru gani hiyo? Ungana na Assumpta Massoi kwa ripoti kamili:

Soundbite 1: Play then hold under

Azimio la UM kwa UNEP ni la kihistoria na linatoa fursa zaidi kwa wanachama wa UM: Steiner

Mwezi Disemba mwaka 2012 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kuhusuu shirika lake linalohusika na mazingira, UNEP. Je azimio hilo lina malengo yapi na manufaa yake ni nini? Tujiunge na Monica Morara.

"We now take a decision on draft resolution entitled, Report of the Governing Council of the United Nations Environment Programme …. The Second Committee adopted the resolution without a vote. May I take it that the assembly wishes to do likewise? It is so decided."

Kampuni ya sukari ya Mumias nchini Kenya na uhifadhi wa mazingira

Harakati za viwanda kujaribu kuhifadhi mazingira kwa kutumia mabaki ya malighafi za bidhaa zake kuzalisha bidhaa nyingine zinazidi kushika kasi, na viwanda kuwa mifano kwa viwanda vingine kama njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira huku zikijiibulia huduma zingine. Miongoni mwa viwanda hivyo ni kile cha sukari cha Mumias nchini Kenya ambacho sasa kinazalisha umeme kwa kutumia rojo zito la sukari, ambayo ni mabaki yatokanayo na uzalishaji wa bidhaa yake, Sukari. Assumpta Massoi na ripoti kamili:

(SAUTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Vita dhidi ya Malaria yakwamishwa na pesa: Tanzania Zanzibar, Rwanda na Zambia zang’ara katika kutokomeza Malaria

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO kuhusu ugonjwa wa Malaria kwa mwaka 2012 imeonyesha kupungua kwa ufadhili katika mipango ya vita dhidi ya ugonjwa huo uliosababisha vifo vya watu takribani Laki Sita na Elfu Sitini duniani kote.

Idadi kubwa ya vifo hivyo ni vya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano. Hata hivyo ripoti hiyo inaonyesha mafanikio katika baadhi ya nchi mathalani Tanzania upande wa Zanzibar ambapo maambukizi kwa sasa ni asilimia Sifuri.

Hofu ya usalama, mila na desturi zakwamisha matumizi ya vyoo

Umaskini pamoja na mila na desturi ni baadhi ya mambo yanayosababisha usafi duni miongoni mwa nchi maskini. Usafi huu duni unamulika zaidi matumizi ya vyoo salama ambapo inaelezwa kuwa kutokana na baadhi ya mila baadhi ya watu wanalazimika kujisaidia haja kubwa vichakani na hivyo kuhatarisha kuenea kwa magojwa kama vile kipindupindu.

Milima yazidi kuporwa, maisha ya wakazi wake yazidi kuwa duni

Milima ni tegemeo la wakazi wa dunia kwa shughuli na huduma mbali mbali ikiwemo maji ya kunywa, umwagiliaji, shughuli za kiuchumi ikiwemo utalii na kadhalika. Hata hivyo maendeleo ya binadamu yamekuwa kikwazo kwa milima kuweza kutoa huduma hizo na hata kuhatarisha maisha ya wakazi au jamii za milimani. Katika siku ya kimataifa ya milima duniani hii leo tarehe 11 Disemba 2012 inaelezwa kuwa milima iko hatarini zaidi hivi sasa na hata maisha ya wakazi wa milimani nayo yanazidi kuwa duni. Je ni kwa nini?