Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 AGOSTI 2022

25 AGOSTI 2022

Pakua

Katika Jarida la Umoja wa Mataifa la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea

-Ni miaka mitano tangu kuzuka kwa mgogoro wa Rohingya nchini Myanmar ambapo mamilioni walilazimika kufungasha virago na wengi kuingia nchini Bangladesh, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema takribani milioni 1 bado ni wakimbii na 150,000 wanaishi makambini Rakhine Bangladesh

-Akiwa amesaliza wiki moja tu kung'atuka madarakani Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet leo akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis amesema amesema  dunia imebadilika kwa kiasi kikubwa na kushuhudia changamoto nyingi kama athari za janga la coronavirus">COVID-19, ongezeko la athari za mabadiliko ya tabianchi, na migogoro mikubwa ya chakula, mafuta na kiuchumi iliyotokana na vita inayoendelea nchini Ukraine.

-Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP David Beasely ameitaka mamlaka ya Tigrayan kurejesha mara moja akiba ya mafuta iliyoibiwa kwa jumuiya ya kibinadamu. 

-Mada kwa kina inatupeleka Mwanza Tanzania ambayo wavuvi wadogo wadogo wamechukua hatua kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kuacha matumizi ya karabai na kugeukia taa za sola

-Katika kujifunza Kiswahili tunaelekera Kenya kwa mtaalam wetu Josephat Gitonga akifafanua maana ya methali "LA KESHO HUONEKANA LEO ILA LA JANA HALIPINGI LA LEO”

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
12'43"