Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 AGOSTI 2022

23 AGOSTI 2022

Pakua

Katika Jarida la habari la Umoja wa Mataifa hii leo , Flora Nducha anakuletea

-Mlipuko mpya wa Ebola wazuka Kivu Kaskazini baada ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 46 kufariki dunia na kuthibitishwa kuwa alikuwa na virusi vya Ebola kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kuwa idadi kubwa ya watoto iko hatarini kupoteza maisha kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji kama kuhara na kipindupindu kwa sababu ya ukame mkali unaoendelea kulikumba eneo la Pembe ya Afrika endap[o hatua hazitochukuliwa

-Wiki ya maji imeanza leo ikibeba maudhui “Kuona yasiyoonekana: Thamani ya maji,” lengo likiwa  kusaidia kuona maji kwa njia mpya na za kuvutia. Kuzingatia thamani ya maji, kutoka kwa mitazamo mingi tofauti ikijikita na mijadala kama vileghrama ya maji, maarifa asilia, haki za binadamu, na mengine mengi.

-Mada yetu kwa kina inajikita na furaha ya Washona ambao kwa mara ya kwanza wamepata haki ya kupiga kura baada ya kupata uraia nchini Kenya

-Na mashinani tunabisha hodi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwa mfanyakazi wa kujitolea ambaye anatumia kila njia kuwafikishia watoto chanjo ya kuokoa maisha katika maeneo ya ndani nchini humo

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
11'33"