Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 AGOSTI 2022

19 AGOSTI 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunamulika siku ya kimataifa ya usaidizi wa binadamu duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatoa shukrani kwa wale wote wanaojitolea kuchukua hatua kusaidia wengine hata wenyewe wakiwa bado na shida, huku akikumbuka wale waliopoteza maisha wakisaidia wengine. Tunakwenda pia Mexico huko ambako taka za mwani zinatengeneza matofali. Makala tunabisha hodi Kigoma, Leah Mushi anakuletea simulizi ya wanawake wanufaika wa miradi inayotekelezwa na UNDP chini ya KJP. Mashinani ni wito kutoka kwa Mkuu wa WHO ili kusaidia wakazi wa jimbo la Tigray nchini Ethiopia. Huduma za msingi hakuna! Mwenyeji wako jaridani leo ni Assumpta Massoi

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'48"