Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

15 Oktoba 2021

Ni Ijumaa ya tarehe 15 mwezi Oktoba mwaka 2021 siku ya kimataifa ya wanawake wa vijijini.

Karibu uungane na Flora Nducha kusikiliza jarida ambapo kama ilivyo ada ijumaa ni siku ya kuwa na mada kwa kina na hii leo tunamulika afya ya akili tukifunga safari hadi Kenya kwa msichana aliyetaka kujiua, kulikoni? 

Pia utapata fursa ya kujifunza lugha ya Kiswahili ambapo leo tunapata ufafanuzi wa maana za neno "KITAMBI" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA.

Sauti
17'31"

14 OKTOBA 2021

Katika Jarida la Habari za UN hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Janga la corona au COVID-19 limerudisha nyuma jitihada za kutokomeza kifua kikuu au Tb limeonya shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO

-Kuelekea siku ya wanawake wa kijijini hapo kesho Oktoba 15 utawasikia wanawake kutoka Tanzania wakielezea changamoto za COVID-19 katika kujikimu kimaisha

-Takwimu mpya zionaonyesha wagonjwa wa COVID-19 wamepungua lakini bado kuna nchi kama Burundi na Korea Kaskazini hazijaanza kutoa chanjo dhidi ya gonjwa hilo

Sauti
15'59"

13 Oktoba 2021

karibu usikilize jarida maalum ambapo leo tunakuletea mada kwa kina tukikupeleka nchini Uingereza kwa mwandishi wa vitabu Abdulrazak Gurnah mshindi wa tuzo ya Nobel ya mwaka 2021 katika fani ya Fasihi. 

Tuzo ya Nobel ilianza kutolewa mwaka 1901 na kamati ya tuzo ya amani ya nobel ya Norway, huwatunukia tuzo pia washindi wengine katika fani za Fizikia, Fiziolojia na madawa, Falsafa, Fasihi na uchumi.

Sauti
15'55"

Jarida 12 Oktoba 2021

Karibu usikilize jarida linaloletwa kwako na Assumpta Massoi ambapo miongoni mwa utakayo sikia ni pamoja na wakulima nchini Kenya wanufaika na mradi wa viazi lishe chini ya ufadhili wa WFP. 

Binti Raba Hakim mkimbizi kutoka Ethiopia aanza masomo ya chuo kikuu kwa ufadhili wa Mastercard Foundation, na nchini Niger wakulima wapewa mafunzo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

Pia utasikia makala na sauti kutokana mashinani.

Sauti
11'32"

11 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida ikiwa leo tarehe 11 mwezi Oktoba mwaka 2021 ni siku ya mtoto wa kike duniani.

Kama ilivyo ada jumatatu ni siku ya mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Tanzania kumulika huduma za posta kwa kutambua kuwa mwishoni mwa wiki ilikuwa siku ya posta duniani. 

Ungana na Flora Nducha anayekuletea jarida 

Sauti
12'13"

08 OKTOBA 2021

Katika jarida la mada kwa kina hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Waandishi wa habari Maria Ressa raia wa Ufilipino na Dimitry Muratov raia wa Urusi wameshinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu 2021

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la mpango wa chakula duniani WFP, la elimu sayansi na utamaduni UNESCO na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wamewapongeza na kuwamwagia sifa washindi hao kwa mchango wao katika kusongeza njia ya amani

Sauti
21'4"

07 OKTOBA 2021

Jaridani hii leo Assumpta Massoi anaanza na taarifa kuhusu umaskini wa kila hali ukimulika hali ya kiafya, kielimu na kiwango cha maisha! Watu wa makabila fulani katika baadhi ya nchi ni hohehahe! Kisha ni taarifa kuhusu uamuzi wa kuruhusu matumizi ya chanjo ya Malaria barani Afrika na bila kusahau leo ni siku ya pamba duniani! Je nguo uliyovaa ni ya pamba? Makala tunabisha hodi Uganda kumulika mradi wa Benki ya Dunia wa ujenzi wa masoko na hatimaye mashinani tukisalia huko huko Uganda na hatua za kujikinga na majanga. Karibu!

Sauti
13'54"

06 OKTOBA 2021

Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea

-Janga la utapiamlo limefurutu ada nchini Afghanistan , huku mabadiliko ya tabianchi na vita vinadhidisha madhila kwa watoto na familia zao yameonya mashirika ya Umoja wa Mataifa la UNICEF na WFP

-Mradi wa uvuvi wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO ujulikanao FISH4ACP baada ya kushamiri Kigoma Tanzania sasa umehamia mkoani Katavi kuwaletea nuru wavuvi

Sauti
14'24"

05 OKTOBA 2021

Katika Jarida la Habari ya Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea 

-Janga la COVID-19 limewaathiri watoto kwa kiasi kikubwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema ni mwiba kwa afya ya akili kwa vijana na watoto

-Leo ni siku ya waalimu duniani UNESCO na wadau wanazihimiza serikali kuwapa waalimu kipaumbele katika kurejesha elimu mahali pake na kurejesha matumaini ya watoto wengi.

Sauti
14'5"

04 OKTOBA 2021

Katika Jarida la Habari hii leo  kutoka Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres akifungua mkutano wa 15 wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendfeleo na biashara UNCTAD15 mjini Bridgetown Barbados ametoa wito wa kuhakikisha usawa wa biashara, uwekezaji na na kujikwamua vyema na COVID-19

-Ripoti ya kamati huru ya uchunguzi wa haki za binadamu nchini Libya imesema kuna ushahidi kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaoweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulitekelewa nchini humo tangu 2016

Sauti
15'10"