Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 OKTOBA 2021

08 OKTOBA 2021

Pakua

Katika jarida la mada kwa kina hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Waandishi wa habari Maria Ressa raia wa Ufilipino na Dimitry Muratov raia wa Urusi wameshinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu 2021

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la mpango wa chakula duniani WFP, la elimu sayansi na utamaduni UNESCO na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wamewapongeza na kuwamwagia sifa washindi hao kwa mchango wao katika kusongeza njia ya amani

-Masda yetu kwa kila leo inatupeleka NASA kwa Dkt. Alinda mashiku ambaye kwa kushirikiana na wenzie wawili wameanzisha wakfu wa kuchagiza wasicha kuingia katika masomo ya sayansi, teknolojia na hisabati STEM amezungumza kwa undani na Idhaa hii

-Na kama ada ya ijumaa ni kujifunza Kiswahili leo tunabisha hodi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania kwa mtaalam Onni Sigalla akifafanua maana ya methali "Zingwizingwi lipe nguo, ulione mashauo"

Audio Credit
UN News/Assumpta Massoi
Audio Duration
21'4"