Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

Jarida 16 September 2021

Katika jarida hii leo utasikia Umoja wa Mataifa umetengeneza darasa maalum katika Makao Makuu yake yaliyoko jijini New York Marekani na kuweka madawati na saa inayoonesha muda ambao wanafunzi wameshindwa kuingia darasani kutokana na janga la ugonjwa wa Corona, COVID-19.

Pia utasikia kuhusu haki za binadamu nchini Burundi. 

Ungana na Assumpta Massoi kusikiliza habari zote kwa undani

Sauti
15'16"

Jarida 15 Septemba 2021

Katika jarida hii leo utasikia jukwaa maalum lililoanzishwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kwa ajili ya elimu ya kung'atwa na nyoka. Nchini Senegal mradi wa kunusuru mikoko umesaidia wavuvi kuongeza kipato na nchini Afghanistan ndege za misaada zaanza kushusha chakula na vifaa vya matibabu. 

Ungana na Assumpta Massoi kwa undani wa taarifa hizo.

Sauti
14'27"

Jarida 14 Septemba 2021

Hii leo katika jarida tutasikia kuhusu mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75 unaofungwa rasmi hii leo na kufunguliwa kwa mkutano wa 76 au UNGA76. Rais wake mteule Abdulla Shahid kutoka Maldives amehojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa na kusema tumaini ndio limesalia kuwa tegemeo kwa mabilioni ya watu duniani wakati huu wakihaha katikati ya janga la COVID-19, uharibifu wa mazingira, vita na majanga mengineyo. 

kwa habari hiyo na nyingine nyingi ikiwemo sauti kutoka mashinani na makala ungana na Assumpta Massoi 

Sauti
15'6"

Jarida 13 Septemba 2021

Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya juhudi mbalimbali kuhakikisha kuwa jamii za watu wa asili haziondolewi katika ardhi na makazi yao ya asili ,hii ni kwa mujibu wa ibara ya 10 ya azimio la Umoja wa Mataifa juu ya haki za watu wa asili la mwaka 2007.

Sauti
11'20"

Jarida 10 Septemba 2021

Leo ni siku ya kuzuia kujiua duniani inayoadhimishwa tarehe 10 Septemba kila mwaka ambapo mwaka huu katika kuhakikisha dunia inashughulikia suala hili la afya ya umma kwa dharura Jumuiya za kimataifa zinakutana kujadili kwa pamoja namna bora ya “kuleta matumaini kwa njia ya vitendo”. 

Lakini kama ilivyo ada ya kila ijumaa tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tutaelekea mkoani Kigoma, Tanzania kusikia namna athari za mabadiliko ya tabianchi zinavyowaathiri wadau wa uvuvi katika Ziwa Tanganyika.
 

Sauti
11'30"

Jarida 09 Septemba 2021

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda maeneo ya shule dhidi ya mashambulizi, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekemea tabia ya makundi yanayopigana kuvamia maeneo ya shule, kukamata watu mateka  na vikosi vya ulinzi kufanya maeneo ya shule kama sehemu zao za kuweka kambi za mapigano. 

Ungana na Flora Nducha kusikiliza habari hiyo na nyingine nyingi.

Sauti
13'

Jarida 08 Septemba 2021

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kujua kusoma na kuandika leo Septemba 8 Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO linasema kumekuwa na hatua kubwa katika miongo kadhaa iliyopita takwimu za mwaka 2019 zikionesha kwamba asilimia 86 ya watu kote ulimwenguni wana uwezo wa kusoma na kuandika ikilinganishwa na asilimia 68 mwaka 1979. 

Pia utasikia mengine mengi ikiwemo elimu kwa watoto wakimbizi na msaada wa kisaikolojia kwa watoto walio kwenye mizozo. 

 

Sauti
13'26"

Jarida 07 Septemba 2021

Hii leo katika jarida utasikia juhudi za mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwenye kusaidia wananchi wa Ethiopia, Haiti na Msumbiji. 

Pia utasikia makala kutoka Uganda kuhusu magonjwa ya mlipuko. 

Sauti
12'13"

Jarida Septemba 03 2021

Katika jarida hii leo utasikia mahojiano na waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Liberata Mulamula ambaye amefanya ziara maalum katika Umoja wa Mataifa. Katika mazungumzo yake na Leah Mushi alianza kwa kumuuliza iwapo iwapo rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan atashiriki katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linaloanza tarehe 21 mpaka 27 Septemba 2021.

kwenye kujifunza Kiswahili leo Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, la ZANZIBAR, BAKIZA, Dkt.Mwanahija Ali Juma anafafanua maana ya maneno "PEMBUA, NYAMBUA NA CHAGUA.

Sauti
12'20"

Jarida Septemba 02 2021

Katika jarida hii leo utasikia ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO iliyotolewa hii mjini Geneva, Uswisi yenye jina 'Hali ya ulimwengu kuhusu hatua za afya ya umma dhidi ya tatizo la kusahau',  inasema ni robo tu ya nchi zote ulimwenguni ambazo zina sera, mkakati au mpango wa kitaifa wa kusaidia watu walio na ugonjwa wa shida ya akili unaosababisha kupoteza kumbukumbu na hali nyingine kama kushindwa kufikiria vizuri.

Kwa habari hiyo na nyingine nyingi ungana na Grace Kaneiya 

Sauti
13'14"