Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 13 Septemba 2021

Jarida 13 Septemba 2021

Pakua

Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya juhudi mbalimbali kuhakikisha kuwa jamii za watu wa asili haziondolewi katika ardhi na makazi yao ya asili ,hii ni kwa mujibu wa ibara ya 10 ya azimio la Umoja wa Mataifa juu ya haki za watu wa asili la mwaka 2007.

Katika Mada kwa kina hii leo tutaelekea nchini DRC kwa walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT 08 wanaohudumu katika Brigedi ya kujibu mashambulizi, FIB ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DR Congo FIB MONUSCO jimboni KIVU Kaskazini ambao wametembelea watu wa jamii ya Mbuti waliokimbia makazi yao na sasa wanaishi katika Kambi ya Kelekele-Mbau Wilaya ya BENI na kutoa misaada mbalimbali kama vile Mavazi na chakula.

Pia utasikia Habari kwa ufupi zikigusia masuala mbalimbali ya misaada ya kibinadamu, Ulinzi wa amani na uchaguzi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'20"