Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

15 APRILI 2021

Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika watia saini makubaliano ya kusongesha mkataba wa biashara huru barani Afrika ulioanza kutekelezwa rasmi mwaka huu wa 2021

-Nchini Burkina Faso adha ya wazazi wanawake kushindwa kufanyakazi kutokana na kukosa walezi wa watoto imepata dawa baada ya Benki ya Dunia na UNICEF kuanzisha mradi wa vituo vya kulelea watoto

Sauti
14'41"
©UNHCR/Ruben Salgado Escudero

14 Aprili 2021

Takribani nusu ya wanawake wote katika nchi zinazoendelea, wananyimwa uhuru wao wa mwili, imesema ripoti ya UNFPA.

Kwa sababu ya COVID-19 Ramadhan mwaka huu itakuwa ngumu sana kwangu, anasema mkimbizi Anna anayeishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mbera nchini Mauritania.

Na FAO yatumia msemo wa tahadhari kabla ya hatari kunusuru mali na uhai Bangladesh.

Sauti
13'2"

13 Aprili 2021

Covid-19 imeongeza ugumu katika mapambano dhidi ya Chagas inayoua takribani watu 10,000 kila mwaka.

UNICEF Sudan Kusini yamletea nuru Adut aliyekuwa hoi taaban.

Na mradi wa FAO wa uhimilishaji ng’ombe nchini Syria ni  nuru katikati ya giza. 

Sauti
11'53"

12 Aprili 2021

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, kwa kushirikiana na mamlaka nchini Colombia wanatumia kila njia ikiwemo ya kutembea nyumba kwa nyumba ili kuwafikia watu wa jamii za asili walio katika mazingira magumu katika eneo la Amazon kusini mwa nchi ambao ni miongoni mwa makundi ya kipaumbele ya kupatiwa chanjo ya COVID-19.

 

Sauti
10'59"

09 Aprili 2021

Wakati ikiwa ni chini ya miaka kumi kufikia ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs mwaka 2030. Kazi bado inaendelea huku pengo katika usawa wa kijinsia ambalo ni lengo namba tano likijitokeza hususan wakati huu wa janga la virusi vya corona au COVID-19.

Sauti
11'22"

07 Aprili 2021

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameueleza ulimwengu uzingatie tulichojifunza kutokana na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.

Wakimbizi kutoka Cabo Delgado wana kiwewe kufuatia walichoshuhudia, limeeleza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Na kuelekea michezo ya majira ya joto ya olimpiki mwaka 2020 itakayofanyika huko Tokyo Japan kuanzia mwezi Julai mwaka huu, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limezindua kampeni ya #TheJourney.
 

Sauti
11'47"

06 Aprili 2021

Mtu mmoja kati ya 3 DRC anakabiliwa na njaa kali, wengi wategemea mzizi Taro.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema, "Tutumie siku ya afya duniani kuboresha mifumo ya afya."

Wanafunzi wakimbizi Iraq wanufaika na ubunifu wa Mwalimu wakati wa COVID-19.

Na mashinani ni harakati za kuweka mazingira bora kati ya wanyama na binadamu nchinI Uganda.    

Sauti
12'28"

05 APRILI 2021

Ugonjwa wa Corona au COVID-19 ulizua zahma kubwa duniani ulipoibuka mwaka jana na kuleta sintofahamu. Hali hiyo bado haijaisha hadi sasa ambapo ni mwaka mmoja umeshapita na watu zaidi ya milioni 128 wameugua duniani kote hadi sasa na kati yao hao zaidi ya milioni 2.8 wamefariki dunia. Bado mazuio ya safari yamewekwa katika baadhi ya nchi na masharti ya kujikinga kwa kuvaa barakoa, kuepuka michangamano na kutumia vitakasa mikono zinazingatiwa. Hata hivyo chanjo imepatikana na inaleta nuru.

Sauti
10'51"

1 Aprili 2021

UNHCR yafanikisha kuwapa hifadhi tena wakimbizi wa Mali waliofurushwa katika kambi Burkina Faso. 

Viongozi wa dini na wananchi wa Mutwanga DRC, wapongeza juhudi za UN kurejesha amani katika eneo lao. 

Mradi wa Benki ya Dunia Afghanistan wasaidia wanawake kuinua maisha yao.

Sauti
12'10"