Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 Aprili 2021

09 Aprili 2021

Pakua

Wakati ikiwa ni chini ya miaka kumi kufikia ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs mwaka 2030. Kazi bado inaendelea huku pengo katika usawa wa kijinsia ambalo ni lengo namba tano likijitokeza hususan wakati huu wa janga la virusi vya corona au COVID-19.

Ushahidi ulio dhahiri kuhusu ukosefu wa usawa ni kumbusho kwa jamii kuhusu umuhimu wa kushirikisha wanawake ikiwemo katika nafasi za kufanya maamuzi katika maisha ya umma na pia utokomezaji wa ukatili kwa ajili ya kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wasichana na wanawake. Jamii kwa kutambua umuhimu wa usawa wa kijinsia pia zinashirikia katika kurekebisha hilo kama inavyoafiki makala hii ya Mathias Tooko wa radio washirika Loliondo FM ya wilaya ya Ngorongoro, mkoa wa Arusha nchini Tanzania.

Audio Credit
Grace Kaneiya
Audio Duration
11'22"