Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

05 APRILI 2021

05 APRILI 2021

Pakua

Ugonjwa wa Corona au COVID-19 ulizua zahma kubwa duniani ulipoibuka mwaka jana na kuleta sintofahamu. Hali hiyo bado haijaisha hadi sasa ambapo ni mwaka mmoja umeshapita na watu zaidi ya milioni 128 wameugua duniani kote hadi sasa na kati yao hao zaidi ya milioni 2.8 wamefariki dunia. Bado mazuio ya safari yamewekwa katika baadhi ya nchi na masharti ya kujikinga kwa kuvaa barakoa, kuepuka michangamano na kutumia vitakasa mikono zinazingatiwa. Hata hivyo chanjo imepatikana na inaleta nuru. Siyo tu kwa wananchi wa kawaida bali pia kwa wahudumu wa afya ambao nao waliingiwa na hofu kama inavyofafanua mada hii inayoletwa kwako na John Kibego mwandishi wetu kutoka Uganda.

Audio Credit
Grace Kaneiya
Audio Duration
10'51"