24 JUNI 2020

24 Juni 2020

Katika Jarida la Umoja wa Matafa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameiasa dunia kufuata katiba ya Umoja wa Mataifa inayotimiza miaka 75 wiki hii katika kutatua changamoto za dunia ikiwemo janga la COVID-19

-Nchini Tanzania hospitali ya CCBRT ambayo ina asilimia 6 ya wahudumu wake wenye ulemavu imesema inachukua hatua zote kuwalinda dhidi ya COVID-19 na kutaka serikali kuweka miundombinu ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wakati wa janga la COVID-19

-Huko Libya mkimbizi kutoka Eritrea mwenye kipaji cha sanaa ya uchoraji apata nuru wakati huu wa COVID-19

-Makala yetu leo iko Uganda kuangazia mkimbizi mfanyabiashara kutoka Rwanda anavyopambana na athari za COVID-19 katika biashara yake

-Na mashinani  utamsikia mchuuzi wa sokoni Wandegeya nchini Uganda akizungumzia msaada wa UNICEF kuwalinda na mbu wakati huu wakilazimika kulala sokoni kulinda familia zao dhidi ya COVID-19

Audio Credit:
UN News /Flora Nducha
Audio Duration:
12'43"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud