Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 JUNI 2020

30 JUNI 2020

Pakua

Leo ni siku ya mabunge duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku muhimu ya kutambua mchango muhimu wa mabunge katika kupaza sauti za wananchi na pia kushawishi uundaji wa sera. Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la idadi ya watu duniani UNFPA imesema ili kukabiliana na janga la kimyakimya la mila potofu hatua za haraka zinahitajika kukomesha ukeketaji (FGM), ndoa za utotoni na mila zingine ambazo zinathiri wanawake na wasichana. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limetoa wito kwa mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ziimarishe uwepo wa jeshi na polisi kwenye maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo ili kunusuru maisha ya raia wanaoendelea kuteseka na kuuawa na vikundi vilivyojihami.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'1"