22 JUNI 2020

22 Juni 2020

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-UNADS yaonya kwamba hatua zisipochukuliwa sasa nchi za kipato cha chini na cha Wastani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara zitaathirika zaidi na COVID-19 hasa kwa wagonjwa wa HIV wanaohitaji dawa za kupunguza makali ya ukimwi

-Nchini Kenya katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma kutana na muhubiri anayetumia kipawa chake kuelimisha wakimbizi na jamii inayowahifadhi kuhusu janga la COVID-19

-Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed ametoa wito binafsi maalum kwa wanaume na wavulana kujiunga na hatua za kukomesha ukatili wa kijinsia na kingono

-Makala yetu leo iko UNEP Tanzania kumulika janga la COVID-19 na mazingira

-Na mashinani tunabisha hodi Malawi utamsikia mzee ambaye mradi wa serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ulivyonufaisha familia yake.

Audio Credit:
UN News/Flora Nducha
Audio Duration:
12'46"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud