Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia bado ipo hatarini kuwa na ongezeko la joto : UNEP

Dunia bado ipo hatarini kuwa na ongezeko la joto : UNEP

Pakua

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP imeeleza kuwa ahadi mpya na zilizorekebishwa kuhusu viwango vya nchi vya kukabili mabadiliko ya tabianchi, NDCs hazijafikia lengo lililowekwa katika mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi na hivyo ulimwenguni kuwa hatarini kuwa na ongezeko la joto la angalau nyuzijoto angalau 2.7 katika karne hii
 
(Leah Mushi na taarifa zaidi.)
Ripoti hiyo ya 12 ikipatiwa jina la “Ripoti ya Pengo la Utoaji hewa chafuzi mwaka  2021: Joto Linaongezeka” imetolewa leo jijini Nairobi, Kenya ikiwa ni siku chache kuelekea katika mkutano wa 26 nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP Inger Andersen amesema "dunia inapaswa kuamka na kuondokana na hatari inayotukabili. Mataifa yanahitaji kuweka sera ili kutimiza ahadi zao mpya, na kuanza kuzitekeleza ndani ya miezi kadhaa. Yanahitaji kufanya ahadi zao za kutozalisha kabisa hewa chafuzi ziwe thabiti zaidi, kuhakikisha ahadi hizi zinajumuishwa katika viwango vya nchi vya kuchangia kukabili mabadiliko ya tabianchi (NDCs), na hatua zinaletwa mbele. Kisha wanahitaji kupata sera ili kuunga mkono azma hii iliyoibuliwa na tena, kuanza kuzitekeleza kwa haraka.”

TAGS: UNEP, Tabianchi na Mazingira, Malengo ya Maendeleo Endelevu, NDCs

 

Audio Credit
Assumpta Massoi / Leah Mushi
Audio Duration
1'17"
Photo Credit
© Unsplash