Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi wa DRC aeleza alivyojikombia kiuchumi

Mkimbizi wa DRC aeleza alivyojikombia kiuchumi

Pakua

Kutana na mkimbizi Felicitee Anibati kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo ambaye kwa sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu nchini Sudan Kusini , ni mama, mkulima na mjasiriamali mwenye mafanikio ambaye sasa anatumia mafanikio yake kuwasaidia wanawake wenzie ili kufika alipo yeye. Flora Nducha anasimulia zaidi

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
Felicitee akiwa kambini Makpandu nchini Sudfan Kusini ambako anasema aliwasili mwaka 2018 kama mkimbizi na alipenda sana kilimo, mwaka jana alianza kulima mahindi na akafanikiwa kuvuna gunia 9 ambapo aliuza magunia 4 na yaliyosalia yalimfaa kwa chakula na familia yake.

Baada ya kupitia madhila mengi ya vita Felicitee amebwaga moyo wake hapa kambini na faida aliyoipata baada ya kuuza mavuno yake akaamua kuanzisha biashara ya ujasiriamali ya ufundi cherahani unaomfaa yeye na wanawake wenzie

“Nilinunua pia cherahani na nimejenga pia nyumba tatu kwa kutumia fedha ninazopata. Na hela kidogo iliyosalia nikaanzisha kikundi cha wanawake ambao sasa tunashona pamoja. Tunanunua vitambaa na kushona nguo ambazo tunaziuza.”

Hakuishia hapo akiba inayopatikana Felicitee anaitumia kuwasaidia wanawake wengi zaidi kupitia bekari ya kuoka na kupika vitu mbalimbali yakiwemo maandazi na hatua hiyo anasema  

Felicitee anaishukuru sana jamii inayomuhifadhi yeye na wakimbizi wengine kwani anasema bila upendo na ushirikiano wao asingeweza kuwa alipo, lakini pia analishukuru shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo linahakikisha wakimbizi wanapata fursa popote walipo.

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Flora Nducha
Audio Duration
2'9"
Photo Credit
Picha na UNICEF/Vockel