Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN

Mafuriko yawatesa wakazi wa White Nile nchini Sudan

Tumeishi hapa tangu miaka ya 1950 na katu hatujawahi kushuhudia mafuriko kama haya, amesema mkazi wa jimbo la White Nile nchini Sudan ambako mafuriko makubwa yamesababisha wakimbizi wa ndani kusaka hifadhi kwa wenyeji wao huku shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wakiendelea kusambaza misaada ya kibinadamu.

Sauti
2'2"
Photo: UNESCO/M. Ravassard

Siku ya Kiswahili duniani ni Julai 7: UN

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO leo limeitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Leah Mushi na taarifa zaidi

Taarifa hiyo imetangazwa leo kwenye makao makuu ya UNESCO mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wan chi wanachama wa shirika hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa twitter wa UNESCO azimio maalum la kuitangaza siku hiyo limepitishwa na wanachama wote bila kupungwa.

Sauti
53"
© UNHCR/Guerchom Ndebo

UNICEF yawaunganisha watoto waliopotea nchini DRC na familia zao

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa zaidi ya miezi sita sasa limeendelea kuwatafuta na kuwaunganisha wazazi, walezi pamoja na maelfu ya watoto waliopoteza wakati wakikimbia usiku baada ya kutokea mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC.

Leah Mushi anasimulia mkasa wa watoto wawili Justin na Justine.

Sauti
2'22"
MINUSCA/Noella Nyaisanga

walinda amani wa Tanzania nchini CAR watoa msaada wa Madarasa na madawati

Mbali na jukumu la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Africa ya Kati CAR, kikosi cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 4 kinachohudumu chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa ujulikanao kama MINUSCA nchini humo , kimeweka mikakati ya kusaidia na kuinua wananchi  wa CAR kielimu kupitia shughuli mbalimbali.

Luteni Noela Julius Nyaisangah afisa habrari wa kisoki hicho anafafanua zaidi katika taarifa hii 

Sauti
2'9"
© WFP/Claire Nevill

Mafunzo ya WFP yamsaidia mkulima kulima mazao mengi na kutafuta wateja kidigitali na kujiongezea kipato zaidi

Kutana na mkulima Mainner mwenye umri wa miaka 44 , ni mama wa watoto wanne na miongoni mwa wakulima wadogo wadogo 150,000 wanaosaidiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kupitia mradi wa kuboresha maisha ya wakulima na kuwajengea mneno, mradi ambao kwake na familia yake umekuwa neema kubwa.

Taarifa ya Flora Nducha na taarifa zaidi 

Sauti
2'25"
© UNICEF/Raphael Pouget

Watoto wanaamini dunia inakuwa bora zaidi huku watu wazima wakiwa na shaka na shuku

Kura ya maoni iliyoendeshwa katika nchi 21 ikihusisha watoto na watu wazima zaidi ya 21,000 imeonesha kuwa watoto wanaamini dunia inakuwa bora zaidi huku watu wazima wakiwa na shaka na shuku.

Taarifa zaidi na Anold Kayanda

Matokeo ya utafiti huo ulioratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, yametolewa leo kuelekea siku  ya mtoto duniani tarehe 20 mwezi huu wa Novemba ambapo watoto na vijana wanaamini kuwa maisha yao ya utoto yamekuwa bora kuliko ya wazazi wao sambamba na huduma za afya na elimu.

Sauti
2'6"
© UNICEF/Jose Vilca

Dawa ya kutibu COVID19 kuuzwa kwa bei nafuu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kwa gharama,  nafuu, UNITAID, leo limetangaza makubaliano ya kuwezesha dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona, COVID-19 kutoka kampuni ya Pfizer ipatikane kwa gharama nafuu kwa nchi za kipato cha chini na kati. 

Taarifa ya Anold Kayanda

Sauti
1'57"
Unsplash/Fotografierende

Wavutaji tumbaku wapungua duniani

Ripoti mpya ya mwenendo wa matumizi ya tumbaku iliyotolewa leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO inaonesha idadi ya watumiaji wa bidhaa za tumbaku duniani imepungua kwa zaidi ya watu milioni mbili tangu mwaka 2015 na inatarajiwa kupungua zaidi ifikapo mwaka 2025. 

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya nne ya mwenendo wa matumizi ya bidhaa za tumbani duniani, mwaka 2015 watumiaji walikuwa bilioni 1.32 na sasa ni bilioni 1.30 huku ifdadi hiyo ikitarajiwa kushuka hadi bilioni 1.27 ifikapo mwaka 2025. 

Sauti
2'48"
CIFOR/Ollivier Girard

Mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zaleta uhasama baina ya wakulima wavuvi na wafugaji

Wakati Mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya Tabianchi COP26 ukiwa umemalizika mwishoni mwa wiki huko Scotland huku Afrika ikisema haijafanikiwa ilivyotaraji, huko nchini Cameroon mabadiliko ya tabianchi yameleta uhasama baina ya wafugaji, wakulima na wavuvi, sababu kubwa ya ugonvi huo ni mbinu walizobuni za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
2'44"
ADB/Al Benavente

UNHCR yasaidia wanajamii wa Sama Bajau kupata vyeti vyakuzaliwa

Cheti cha kuzaliwa ni moja ya nyaraka muhimu kwa utambulisho wa mtu, lakini pia kigezo cha kusaidia kupata huduma za msingi kama za afya, elimu na hata hifadhi ya jamii.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mambo ni tofauti sana kwa jamii ya wavuvi ya Sama Bajau inayoishi kwenye mwambao wa Ufilipino, Malaysia na Indonesia ambao kwa miaka mingi wamekosa huduma kwa kutokuwa na vyetu vya kuzaliwa na hivyo kukosa utaifa.

Sauti
2'29"