Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

walinda amani wa Tanzania nchini CAR watoa msaada wa Madarasa na madawati

walinda amani wa Tanzania nchini CAR watoa msaada wa Madarasa na madawati

Pakua

Mbali na jukumu la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Africa ya Kati CAR, kikosi cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 4 kinachohudumu chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa ujulikanao kama MINUSCA nchini humo , kimeweka mikakati ya kusaidia na kuinua wananchi  wa CAR kielimu kupitia shughuli mbalimbali.

Luteni Noela Julius Nyaisangah afisa habrari wa kisoki hicho anafafanua zaidi katika taarifa hii 

Natsss….. 
Katika mkoa wa wa Mambere Kadei  wilaya ya Berberati, sambamba na kutoa ulinzi kwa wananchi TANBAT 4 imekuwa mdau mkubwa wa kusaidia wananchi katika shughuli za kijamii na hivi karibuni wamejenga na kukabidhi vyumba viwili vya madarasa na vifaa vya kufundishia ikiwemo ubao kwa kila darasa na madawati 100. 
Vifaa hivyo na madarasa vimekabidhiwa katika shule ya msingi ya kikatoliki ya Secret Heart of Jesus mkoani humo.  

TANBAT4 inasema kukamilika kwa madarasa hayo  kama sehemu ya maendeleo ya miundombinu nchini  CAR yatasaidia shule kuongeza wanafunzi 100 zaidi kwa kila muhula. 

Hafla ya kukabidhi madarasa hayo na vifaa  ilihudhuriwa na Kamanda wa kikosi cha MINUSCA Luteni Jenerali Daniel Sidiki Traore, Balozi wa Tanzania nchini CAR Luteni Jenerali mstaafu Paul Ignace Mella, Askofu wa Dayosisi ya Berberati, askofu Dennis Kofi Agbenyadzi pamoja na mamlaka za utawala wa mkoa wa Mambere Kadei. 

Kamanda kikosi wa MINUSCA aliwapongeza TANBAT4 kwa juhudi  zao kwenye kufanikisha ujenzi huo 
 
Naye Balozi wa Tanzania Luteni Jenerali mstaafu Paul Ignace Mella aliongezea kwa kusema 
 
Mwasham Askofu pamoja na mamlaka za utawala wa mkoa wa Mambere Kadei walitoa shukrani zao za dhati kwa TANBAT4 na MINUSCA kwa ujumla kwa mchango wao wa  kuinua elimu nchini CAR.

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Noela Julius Nyaisangah
Sauti
2'9"
Photo Credit
MINUSCA/Noella Nyaisanga