Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wavutaji tumbaku wapungua duniani

Wavutaji tumbaku wapungua duniani

Pakua

Ripoti mpya ya mwenendo wa matumizi ya tumbaku iliyotolewa leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO inaonesha idadi ya watumiaji wa bidhaa za tumbaku duniani imepungua kwa zaidi ya watu milioni mbili tangu mwaka 2015 na inatarajiwa kupungua zaidi ifikapo mwaka 2025. 

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya nne ya mwenendo wa matumizi ya bidhaa za tumbani duniani, mwaka 2015 watumiaji walikuwa bilioni 1.32 na sasa ni bilioni 1.30 huku ifdadi hiyo ikitarajiwa kushuka hadi bilioni 1.27 ifikapo mwaka 2025. 

Nchi 60 zimetajwa kuwa mbioni kutimiza lengo la hiyari la kimataifa la kupunguza kwa asilimia 30 matumizi ya tumbaku kati yam waka 2010 na 2025 ikiwa ni ongezeko kutoka nchi 32 miaka miwili iliyopita. 

WHO imesema maisha ya mamilioni ya watu yameokolewa kwa kuwa na sera madhubutio na zenye ufanisi za kudhibiti matumizi ya bidhaa za tumbaku chini ya mkakati wa WHO FCTC na MPOWER na hay ani mafanikio makubwa katika vita dhidi ya uraibu wa tumbaku. 

Akizungumzia mafanikio hayo mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedross Adhanom Ghebreyesus anesema “Inatia moyo sana kuona kwamba watu wachache wanatumia bidhaa za tumbaku kila mwaka na nchi nyingi ziko mbioni kufikia malengo ya kimataifa.Hata hivyo bado safari bado ni ndefu na makampuni ya tumbaku yataendelea kutumia kila mbinu kutetea faida kubwa wanayoipata kwa kuuza bidhaa hizo hatari. Tunazichagiza nchi zote kutumia nyenzo bora zilizopo kusaidia watu kuacha matumizi ya tumbaku na kuokoa maisha.” 

Ripoti pia imezitaka nchi kusongesha mchakato wa utekelezaji wa hatua zilizoorodheshwa kwenye makakati wa WHO wa FCTC ili kuendelea kupunguza idadi ya watu walio hatarini kuugua au kufa kutokana na magonjwa yanayochangiwa na matumizi ya tumbaku.
 
Ripoti imebaini kwamba kwa mwaka 2020 asilimia 22.3 ya watu wote duniani walitumia bidhaa za tumbaku, asilimia 36.7 kati yao ni wanaumee huku silimia 7.8 wanawake. 

Kwa upande wa watoto ripoti imesema kuwa “takriban asilimia 38 ya watoto wa umri wa miaka kati ya 13-15 hivi sasa wanatumia bidhaa za tumbaku milioni 13 wakiwa ni wasichana na milioni 25 wavulana.” 

Kwa mujibu wa ripoti uunguzo la kiasi kikubwa la matumizi ya tumbaku linashuhudia katika nchi za Amerika wakati barani Afrika ndiko kuliko na kiwango cha chini zaidi cha matumizi ya bidhaa za tumbaku.

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Flora Nducha
Audio Duration
2'48"
Photo Credit
Unsplash/Fotografierende