Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

©MONUSCO/FIB/Mohammed Mkumba

JWTZ na mipango yao ili utendaji wao uendane zaidi na mazingira. T

Wakati Tanzania ikijiandaa kupeleka kikosi chake katika vikundi vipya vitakavyokuwa na uwezo wa kuchukua hatua haraka zaidi kukabiliana na vitisho na hatimaye kuimarisha ulinzi wa raia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC , chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa, mkuu wa mafunzo na utendaji wa kivita wa jeshi la wananchi wa Tanzania, JWTZ amezungumzia kile ambacho watafanya ili utendaji wao uendane zaidi na mazingira. Tupate maelezo zaidi kutoka Luteni Issa Mwakalambo Afisa habari wa kikosi cha 7 cha Tanzania kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi.

Sauti
4'13"
UN Photo/Rick Bajornas)

UNICEF na wadau nchini Malawi mstari wa mbele kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata elimu juu ya COVID-19

Janga la ugonjwa wa Corona, COVID-19 likiendelea kushika kasi katika baadhi ya nchi, Umoja wa Mataifa nao kupitia shirika lake la kuhudumia watoto UNICEF nchini Malawi pamoja na wadau, wamechukua hatua kuhakikisha kuwa watoto wenye ulemavu hawaachwi nyuma katika kupata elimu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.

Sauti
2'12"
UN Tanzania

FUWAVITA, daraja kwa wanawake wenye ulemavu kupata stadi nchini Tanzania

Nchini Tanzania, taasisi ya FUWAVITA yaani Furaha ya Wanawake Viziwi Tanzania imekuwa ikiwawezesha wanawake wenye ulemavu nchini humo hususani wanawake viziwi kupata stadi za uongozi na ujasiriamali. Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa amemhoji mwanzilishi wa taasisi hiyo, Aneth Gerana Isaya kupitia mkalimani wa lugha ya ishara Bwana Billbosco Muna. 

Sauti
2'
© UNICEF/Tanya Bindra

Mwanaharakati wa hisibati, kulikoni?

Dunia inakuwa mahali bora pa kuishi ikiwa kila mtu atachangia katika kutaka hali hiyo itokee. Kutana na Yusuf Adamu Ibrahim, mwanaharakati mchanga wa hisabati kutoka jimbo la Bauchi, Nigeria ambaye anabadilisha maisha ya watoto wa shule katika jamii yake kwa kuwasaidia kuboresha ujuzi wao wa hesabu. Yusuf ni hamasa kwa wengi, na ni kijana mdogo wa umri wa miaka 18 mpenda mabadiliko.

Sauti
2'21"
UN Photo/David Mutua

Dunia inahitaji kuchukua hatua zaidi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi-UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, kesho Jumatano likifanya mkutano wa ngazi ya juu kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa wakimbizi na wakimbizi wa ndani, pamoja na wengine walio katika mazingira hatarishi kote, mshauri maalumu wa UNHCR kuhusu mabadiliko ya tabianchi Andrew Harper amesema dunia inapaswa kuchukua hatua kali zaidi kwani mabadiliko ya tabia nchi huwezi kuyavalia barakoa. 

Sauti
1'49"