15 JANUARI 2020
Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea
-Ripoti mpya iliyotolea na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA inasema hatua za haraka zinahitajika ili kunusuru maisha ya maelfu ya wanawake wajawaziti na watoto wanaozaliwa Darfur Magharibi baada ya kutawanywa na machafuko ya kikabila
-Msimu wa baridi umeelezwa kuongeza madhila zaidi kwa maelfu ya watu Idlib Syria hususan watoto kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF