FAO na WFP kwa pamoja kukabiliana na njaa DRC
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la chakula na kilimo FAO, na la mpango wa chakula WFP yamekusanya nguvu ili kukabiliana na tatizo la njaa katika eneo la Kasai Kuu huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.
Alexis Bonte ambaye ni mwakilishi wa muda wa FAO amesema watatumia kiasi cha dola milioni 10 zilizotolewa na serikali ya Ubelgiji ili kuboresha maisha ya raia laki moja ambao ni wakimbizi wa ndani katika migogoro ya wenyewe kwa wenyewe katika eneo la Kasai.