Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Ugonjwa wa kifua kikuu, changamoto na tiba

Kifua kikuu au TB!Gonjwa lililoorodheshwa na shirika la afya ulimwengni WHO kuwa miongoni mwa magonjwa 10 yanayoongoza kwa kusababisha vifo duniani.

WHO inasema mathalani mwaka 2015 watu milioni 10.4 waliugua ugonjwa huo, milioni 1.8 walifariki duniani, wakiwemo takribari watu Laki tano ambao walikuwa na virusi vya Ukimwi, VVU. Miongoni mwa waathirika ni kundi la wahamiaji ambalo katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani tarehe 24 mwezi Machi, limeangaziwa.

Miili ya wahudumu wa misaada ya kibinadamu kutoka Kenya waliouawa Sudan Kusini kusafirishwa

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohamed Ijumaa ametangaza kwamba miili ya wahudumu wa misaada watatu kutoka Kenya waliouawa mwishoni wa wiki iliyopita nchini Sudan kusini itasafirishwa kesho Jumamosi kutoka Juba na kurejeshwa nyumbani Kenya.

Ubalozi wa Kenya Juba na ubalozi wa Sudan Kusini Nairobi wanashirikiana kuratibu zoezi hilo.

Wahudumu hao ni miongoni mwa wahudumu sita wa misaada ya kibinadamu waliouwa wakisafiri kutoka Juba kuelekea Pibor Jumamosi iliyopita.

Wanamuziki wapazia kilio cha Yemen

Nchini Yemen, mapigano yaliyoanza miaka miwili iliyopita, yamekuwa mwiba siyo tu kwa raia bali pia kwa wale wanaotumia nchi hiyo kama njia ya kupitia kuvuka ghuba ya Aden na bahari ya Sham kwenda nchi nyingine. Wakimbizi na wahamiaji wanakumbwa na majanga kama vile kutekwa, kutumikishwa na hata wengine kukosa chakula na huduma za msingi. Wengine wanakuwa wako safarini kwenda Ulaya lakini kupitia Yemen inakuwa ni pengine mwisho wa ndoto yao.

Muda wa MONUSCO waongezwa hadi 2018, askari wapunguzwa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linaloongeza muda wa ujumbe wa umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO hadi tarehe 31 mwezi Machi mwakani.

Pamoja na kuongeza muda wa ujumbe huo, azimio hilo limegusia suala nyeti lililokuwa linajadiliwa kuhusu kupunguza idadi ya askari, ambapo sasa imepunguzwa hadi askari 16,215.

Azimio limemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kufanya tathmini ya majukumu ya MONUSCO kwa wakati huu kuona iwapo majukumu yote ni muhimu.

Uamuzi wa Israel kuhusu makazi mapya ya walowezi umenisikitisha-Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema amesikitishwa na kutiwa shaka na uamuzi wa Israel wa kujenga makazi mpaya ya Walowezi kwenye eneo linalokaliwa la Wapalestina.

Kupitia ujumbe uliotolewa na msemaji wake Ijumaa, Katibu Mkuu amekuwa akisisitiza kila wakati kwamba hakuna mpango mbadala kwa Waisrael na Wapalestina kuishi pamoja kwa mani na usalama.

Na amelaani hatua zote kama hii ya sasa ambayo inatishia mustakhbali wa amani na suluhu ya kuwa na mataifa mawili.

Wenye usonji wanakosa haki za msingi za binadamu

Kwa kuzingatia haki za msingi za binadamu kwa watu wenye usonji, dunia inaishi kizani , kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya usonji.

Akizungumza Ijumaa katika tukio maalumu la kuadhimisha siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu usonji kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, profesa Simon Baron-Cohen mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa usonji kwenye chuo kikuu cha Cambridge Uingereza , amesema usonji ni ugonjwa wa maisha unaoathiri mishipa na kujitokeza kupitia ulemavu mbalimbali.

Wahamiaji 655 wafariki wakisaka hifadhi-IOM

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM linasema wahamiaji na wakimbizi karibu 700 wamefariki katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu wa 2017 wakati wa safari za kusaka hifadhi sehemu mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo msemaji wa IOM Joel Millman amesema idadi hiyo hata hivyo bado haijavuka ile ya kipindi cha miezi mitatu ya mwaka jana ambapo wahamiaji na wakimbizi 749 walifariki katika kipindi hicho.

Neno la wiki- Misele

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia matumizi yasiyo sahihi ya neno Misele Mchambuzi wetu  Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA anasema neno misele ni aina ya dawa lakini linatumika kumaanisha kutia nakshi lakini hiyo si sahihi kwani hamna usanifu na lnatumika kwa mazoea lakini sio sanifu.

Kupitishwa kwa Baraza la mawaziri Somalia ni hatua chanya- UM

Umoja wa Mataifa umekaribisha hatua ya Bunge la Somalia kupitisha Baraza la Mawaziri lililoteuliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hassan Ali Khaire mapema mwezi huu.

Baraza hilo lina mawaziri 27 ambao sita kati yao ni wanawake, hatua ambayo Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa umoja huo nchini Somalia, Michael Keating amesema ni chanya katika kuwezesha kisiasa wanawake wa nchi hiyo ya pembe ya Afrika.

Idadi hiyo ya wanawake kwenye Baraza la Mawaziri ni kubwa kuwahi kujumuishwa kwenye serikali ya shirikisho Somalia.