Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Dungusi kakati ni jibu la njaa- FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema majani na matunda ya dungusi kakati ni suluhu ya ukosefu wa chakula kwa binadamu na mifugo katika maeneo yenye  ukame.

Ni kwa mantiki hiyo FAO tayari imekutanisha wataalamu ili kubonga bongo kusaidia wakulima na watunga sera juu ya jinsi ya kutumia vema tunda hilo lenye rangi nyekundu ambalo mara nyingi hupuuzwa.

Tumakinike ili tulinde mali za kitamaduni kwenye mizozo- Azoulay

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea ripoti ya utekelezaji wa azimio lake la ambalo pamoja na mambo mengine linalaani uharibifu na usafirishaji wa mali za kitamaduni kwenye eneo yenye vita, kitendo ambacho kinafanywa na vikundi vya kigaidi.

Akiwasilisha ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa shirika Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO Audrey Azoulay amesema kuna nuru katika ulinzi wa mali hizo.

Shule ya Michungwani, Handeni Tanga yapata jibu la utoro kwa wanafunzi

Lengo namba 4 la malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, linapigia chepuo elimu bora. Hii inamaanisha pamoja na mambo mengine watoto siyo tu waandikishwe shule bali pia wamalize masomo yao hadi mwisho bila kukosa.

Hata hivyo utoro unaonekana kuwa ni kikwazo katika baadhi ya nchi na Tanzania ni miongoni mwao. Hata hivyo kwa kutambua changamoto hiyo tayari serikali imeanza kuchukua hatua, mathalani huko wilaya ya Handeni mkoani Tanga, shule ya msingi Michungwani yenye jumla ya wanafunzi 1285.

Tamasha la Kusini-Kusini 2017 lakunja jamvi Uturuki

Tamasha la kimataifa la ushirika wa Kusini-Kusini mwaka 2017 leo limekunja jamvi mjini Antalya Uturuki huku umoja wa Mataifa na wadau wakifurahia matokeo .

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya ushirika wa Kusini-kusini Jorge Chediek, lengo la tamasha hilo ambalo huandaliwa kila mwaka ni kutoa fursa kwa nchi za Kusini -Kusini , taasisi mbalimbali na mataifa mengine yakiwepo ya Kaskazini kujumuika pamoja na kuanzisha ushirika mpya ili kufaidika na ushirika wa Kusini-kusini na kwa mwaka huu amesema lengo limetia na kuongeza kuwa

WFP na UNFPA washirikiana kuokoa barubaru Laos

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwe lile la mpango wa chakula duniani WFP na lile idadi ya watu ulimwenguni UNFPA yameazimia kushirikiana hii leo  katika suala la kuwekeza katika  maendeleo ya vijana barubaru wa kike nchini Laos.

Ushirikiano huo ni kupitia programu iliyobuniwa ikipatiwa jina la Noi ambaye ni msichana barubaru wa Laos akitumika kuelimisha umuhimu wa kuweka mjadala wa wazi na barurabaru wa kike kama njia ya kukabiliana na changamoto wanazopata kundi hilo nchini humo.

Makubaliano ya kimataifa kuhusu uhamiaji yasisahau watoto- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema makubaliano ya kimataifa kuhusu uhamiaji duniani, ni lazima yajumuishe watoto waliolazimika kuondoka makwao kutokana na sababu mbalimbali.

UNICEF imesema hiyo wakati nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wakijiandaa kukutana huko Puerto Vallarta Mexico kuanzia wiki ijayo kuandika rasimu ya makubaliano hayo, na hivyo kuhitimisha takribani mwaka mzima wa majadiliano.

Palestina na Israeli wakae meza moja kumaliza tofauti zao : Guterres

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limekutana leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuonyesha mshikamano na wapalestina, ili kujadili mustakabali wa eneo hilo ambalo limekuwa katika migogoro kwa miongo zaidi ya mitano.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kupitia naibu wake, Amina J. Mohammed, amerejelea wito wake kwa waisreli na wapalestina kukaa meza moja na kutafuta suhulu ya mgogoro uliodumu kwa kipindi kiferu sasa.

Marufuku ya "viroba" Tanzania yaleta nuru kwa vijana

Katika ajenda ya Umoja  wa Mataifa ya  malengo ya  maendeleo endelevu SDGs au ajenda  2030, vijana kama nguvu kazi na mustakabali wa dunia wanapewa jukumu la kijiendeleza ili kujikwamua na suala la umasikini siku za usoni.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika hutuba yake huko Abidjan, Cote D’Ivoire amezieleza  serikali  za Afrika na zile za Ulaya  kwamba ili kufikia  mustakhbali bora ni lazima kuwekeza katika vijana leo.

UNHCR yapongeza hatua ya kuanzishwa kwa makazi ya mpito ya wakimbizi Libya

Shirikia la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limekaribisha uamuzi wa Libya wa kuanzisha kituo cha mpito kwa ajili ya wahamiaji huko Tripoli ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuimarisha ulinzi wa kundi hilo.

Bwana Roberto Mignone ambaye ni mwakilishi wa UNHCR Libya amesema uamuzi huo wa serikali unawatengenezea wakimibizi husuan wanawake na watoto mazingira yalio salama na pia utarahisishia juhudi za UNHCR katika mchakato wa kuwatafutia wakimbizi na wahamiaji makazi ya kudumu.