Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa satellite kufuatilia safari za ndege utaimarisha usalama:ITU

Mfumo wa satellite kufuatilia safari za ndege utaimarisha usalama:ITU

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya habari na teknolojia ya mawasiliano ITU limesema uwezo wa kufuatilia ufanisi, mwenendo na kutoa ripoti za safari za ndege ni muhimu ili kuhakikisha usalama wa abiria na wafanyakazi, pamoja na jamii zilizoko chini.

Shirika hilo linasema ukizingatia kwamba takribani ndege 59,000 zinakuwa safarini hewani kwa wakati mmoja kote duniani viwango vya kupata data bora za kinachoendelea ni lazima. Na kwa mantiki hiyo ITU ambayo ndiyo inayoanzisha viwango vya mifumo mbalimbali ya mawasiliano kote duniani , sasa imepitisha misingi mikuu ya kiufundi ya kuboresha uwezo wa ndege kujitegemea katika kufuatilia kinachoendelea ndani ya ndege hizo na kutoa ripoti kupitia satellite kote duniani.

Ufuatiliaji huo unaojiendesha wenyekwe kwenye ndege ni mbinu ambapo ndege inatoa yenyewe data kutoka kwenye kiongoza mwendo cha ndani ya ndege, na mfumo wa kuonyesha ndege ilipo, ikiwa ni pamoja na kuitambua ndege hiyo katika pande nne mfano, umbali, masafa, inaruka urefu gani na muda lakini pia kutoa taarifa zaidi inapohitajika.

Photo Credit
Mfumo wa satellite kufuatilia safari za ndege ni muhimu kwa kuhakikisha usalama wa abiria. Picha: ITU