Makala Maalum
Habari kwa Picha
Baada ya vita Gaza: Simulizi za wahudumu wa afya
Huku Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel baada ya vita vikali kwa miaka miwili, wafanyakazi wa afya walibeba mzigo mkubwa wa kutoa matibabu na wenyewe wakibaki na kiwewe. Kupitia usaidizi wa ajira za dharura, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP linatoa fursa za ajira katika sekta za afya, elimu na sekta binafsi.
Katika Hospitali ya Al Shifa, kituo kikubwa zaidi cha matibabu na hospitali kuu katika Ukanda wa Gaza, wafanyakazi 610 wamepatiwa ajira za dharura, pamoja na kufanyika kwa ukarabati wa miundombinu na kutoa makazi ya msaada. Je ni yapi waliyopitia watoa huduma za afya katika miaka miwili ya vita ambapo wengine walikuwa wangali wanafunzi? Na ipi ni mipango yao ya baadae mara baada ya kupata ajira kutoka UNDP?