Shule ya msingi Uingereza yafungua milango kwa watoto wakimbizi
Huko nchini Uingereza, shule moja ya msingi imefungua milango yake kwa ajili ya watoto wakimbizi na familia zao. Patrick Newman na ripoti kamili.
(Taarifa ya Patrick Newman)
Jamii inayozunguka shule ya msingi ya Widden huko Gloucester, nchini Uingereza imechukua hatua hiyo na hivyo kuungana na harakati za kugeuza miji kuwa vituo vya hifadhi kwa wakimbizi.
Lengo la mpango huo unaoenda sambamba na makubaliano ya kimataifa kuhusu wahamiaji, ni kuwapatia makazi salama raia wanaokimbia hatari nchini mwao na kusaka eneo salama Uingereza.
Katika muongo mmoja sasa zaidi ya miji 90 imechukua hatua hiyo ambapo shule ya msingi ya Widden imechukua hatua kuonyesha kuwa nguzo ya kujumuisha watu wa mataifa yote.
(Sauti ya Heather Jones)
“Shule ya hifadhi ni shule ambamo kwayo tunataka watoto wafahamu kuwa wako salama, hasa pale wanapokuwa wametoka maeneo yasiyo salama.”