Mtazamo kuhusu uhamiaji unasikitisha- Arbour

18 Disemba 2017

Hii leo ikiwa ni siku ya wahamiaji duniani, Umoja wa Mataifa umetaka kampeni mahsusi ya kubadili mtazamo wa umma kuhusu wahamiaji.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji, Louise Arbour ameieleza Idhaa ya Umoja wa Mataifa kuwa..

(Sauti ya Louise Arbour)

“Katika mazingira mengi watu hudhani wahamiaji ni wanaume tena vijana ambao wanaingia nchini na kuchukua ajira za watu au kunufaika na ustawi wa jamii. Ukweli ni tofauti kabisa. Asilimia 48 ya wahamiaji ni wanawake, na wahamiaji hulipwa ujira mdogo sana na huchukua kazi ambazo jamii za wenyeji hawazipendi.”

image
Vijana wakimbizi katika maadhimisho ya siku ya wahamiaji(MAKTABA). Picha: IOM

Hivyo amesema katika siku ile kila mtu aangalie kwenye makazi yake na atambue wahamiaji ni akina nani na mazingira yao yako vipi na kwa upande wa serikali…(Sauti ya Louise Arbour)

“Hili ni eneo ambalo kubadili simulizi na mtazamo wa umma utachukua muda kushawishi viongozi wa kisiasa kuchukua uamuzi sahihi kuhusu uhamiaji kwa maslahi ya jamii zao, wahamiaji na pia kwa manufaa ya nchi zinazoendelea.”

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, uhamiaji umekuwepo tangu zama za kale na na utaendelea kuwepo kwa kuzingatia mazingira mbali mbali ya sasa ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, machafuko, ukosefu wa usawa na hata watu kusaka maisha bora.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter