Hatma ya uhamiaji wa kimataifa; Macho na masikio vyaelekezwa Mexico

4 Disemba 2017

Mkutano wa kuandaa rasimu ya kwanza ya makubaliano ya kimataifa kuhusu uhamiaji unaanza leo huko Puerto Vallarta nchini Mexico, ikielezwa kuwa jambo la msingi ni kuhakikisha makubaliano hayo yanazingatia utofauti wa mahitaji ya wahamiaji kote ulimwenguni.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji wa kimataifa Louise Arbour akizugumza na Idhaa hii amesema ujumbe wake kwa washiriki ni kwamba..

(Sauti ya Louise Arbour)

« Ujumbe ni kwamba iwapo tunataka kuzungumzia makubaliano ya kimataifa, ni lazima uwe wa kimataifa lakini uzingatia mahitaji tofauti ya kikanda. »

Mathalani amesema mahitaji ya wahamiaji barani Asia ni tofauti na mahitaji ya wahamiaji Afrika au barani Ulaya, hivyo amesema lazima serikali zitambue kuwa zinapaswa kutunga sera zinazokidhi mahitaji ya eneo husika.

Akizungumzia matarajio kutoka mkutano huo, Bi. Arbour amesema ni makubwa mno baada ya msururu wa vikao vya kikanda kujadili masuala yanayopaswa kuwepo kwenye makubaliano hayo kwa hivyo..

(Sauti ya Louse Arbour)

«Ni kutoka katika mkutano huu ambapo rasimu ya kwanza ya makubaliano hayo itatoka. Nchi wanachama zitaanza kuelewa maeneo ambayo wanakubaliana, wapi wanajikita zaidi, matumaini na matarajio. Tutakuwa pia katika nafasi nzuri baada ya

huu kuona wapi kazi inapaswa kufanywa zaidi, wapi kuna changamoto zaidi.”

Mchakato wa kikanda ulianza mwezi Aprili hadi Novemba mwaka huu.

image
Picha: Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji wa kimataifa Louise Arbour. UM/Ky Chung

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter